Psalms 82

Maombi Kwa Ajili Ya Kutaka Haki

(Zaburi Ya Asafu)


1 aMungu anaongoza kusanyiko kuu,
anatoa hukumu miongoni mwa “miungu”:


2 b“Hata lini utaendelea kuwatetea wasio haki
na kuonyesha upendeleo kwa waovu?

3 cTeteeni wanyonge na yatima,
tunzeni haki za maskini na walioonewa.

4 Mwokoeni mnyonge na mhitaji,
wakomboeni kutoka mkononi mwa mwovu.


5 d“Hawajui lolote, hawaelewi lolote.
Wanatembea gizani;
misingi yote ya dunia imetikisika.


6 e“Nilisema, ‘Ninyi ni “miungu”;
ninyi nyote ni wana wa Aliye Juu Sana.’

7 fLakini mtakufa kama wanadamu wa kawaida;
mtaanguka kama mtawala mwingine yeyote.”


8 gEe Mungu, inuka uihukumu nchi,
kwa kuwa mataifa yote ni urithi wako.
Copyright information for SwhKC